Categories
Habari Maisha

Kanisa Katoliki Latangaza Kuunga Mkono Ushoga

Katika hatua inayoweza kuzua mtafaruku mkubwa, kiongozi mkuu wa Kanisa la Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Francis, kutamka kuwa ndoa za jinsia moja zilindwe na sheria.

“Mashoga wana haki ya kuwa katika familia. Ni watoto wa Mungu na wana haki ya familia. Haipaswi kumtimua mtu au kumfanya ajisikie vibaya,” aliongea Baba Mtakatifu katika waraka wa video uliopewa jina “Francesco.”

“Zinapaswa kuwepo sheria za mahusiano ya jinsia moja. Katika namna hiyo, zitakuwa zina ulinzi wa kisheria,” alisema.

Chanzo: ABS-CBN News