Categories
Kimataifa

Kamala Harris Kuwa Mwanamke Mmarekani Mweusi Wa Kwanza Kuwa Makamu wa Rais wa Nchi hiyo?

 

Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Democrats Joe Biden amemteua “mpinzani wake wa awali” Kamala Harris kuwa mgombea mwenza wake. Kamala ambaye nae aliwania kuchaguliwa kuwa mpeperusha bendera wa chama hicho kabla ya kujitoa na kumuunga mkono Biden, anaweza kuingia kwenye historia ya taifa hilo kama Mmarekani Mweusi wa kwanza kuwa makamu wa rais wa nchi hito endapo Biden atashinda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo November mwaka huu.

Kamala Harris Is Eyeing Iowa to Reverse Her Summer Slump—but Can That Save  Her Campaign?

Hata hivyo, Kamala anatarajiwa kukabiliana na mashambulizi makali kutoka kwa mpinzani wa Biden, Rais Donald Trump, ambaye licha ya rekodi yake ndefu ya unyanyasaji wanawake, ni mbaguzi wa rangi wa waziwazi. Kadhalika, mwanasiasa huyo anatarajiwa kushambuliwa vikali na wafuasi wa Trump ambapo miongoni mwao ni wenye mrengo mkali wa kulia na wabaguzi wa rangi wa kupindukiz.