Categories
Habari

RC Rukwa Aagiza Wanafunzi Kukaguliwa Kubaini Wanaovaa Hirizi Shuleni

Agizo hilo alilitoa jana kwenye mkutano alioufanya Kijiji cha Malonje wilayani Sumbawanga kutokana na baadhi ya wananchi kudaiwa kuwa na tabia ya kuwaita waganga wa jadi, maarufu lambalamba, na kuwalipa fedha ili wawasafishie nyumba na mali zao.

“Kutokana na baadhi ya wazazi wa wanafunzi kuamini ushirikina kupita kiasi, huenda wakawapa hata watoto wao hirizi na matunguli ili waende nayo shuleni wakiamini kuwa vitu hivyo vitawalinda watoto wao hali ambayo itasababisha usumbufu kwa wanafunzi wengine.

“Walimu wakuu na wakuu wa shule, wakagueni wanafunzi wenu ili muone kama wamevaa hirizi, kwani hayo ndiyo yanayowasumbua wanafunzi wengine, utakuta kwenye shule wanafunzi wanaugua ugonjwa wa kuanguka ovyo, hirizi ndiyo inasababisha hali hiyo,” aliagiza.

Thanks