Categories
Habari

Mitano Tena: Watumishi Namtumbo Wadai Posho Ya Miezi Mitano

WATUMISHI mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo iliyopo Mkoa wa Ruvuma walioshiriki zoezi uandikishaji vyeti vya kuzaliwa vya watoto.wamelalamikia kusotea posho zao kwa zaidi ya miezi mitano sasa .
Watumishi hao wanasema wanadai posho ya zaidi ya Sh milioni 100 na juhudi zao za kuzidai zinaelekea kugonga mwamba.
Pamoja na kudai kuwa hawajalipwa fedha hizo wanasema katika zoezi zima wamelipwa posho ya wiki 2 na hawajalipwa tena.
Walieleza kuwa hata wanapofuatilia malipo hayo kwa uongozi huambiwa wasubiri mpaka watakapoitwa kwa barua na kwamba wamsubiri hadi sasa imepita miezi mitano hawajaitwa wala kuonekana dalili za kulipwa.
Aidha walieleza kuwa kwa taarifa walizonazo ni kwamba fedha hizo zimebadilishiwa matumizi.
Hata hivyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Evans Titus licha ya kukiri watumishi hao kuidai halmashauri hiyo alikanusha taarifa za mabadiliko ya matumizi ya fedha hizo na kwamba
kuchelewa ni sababu za kimfumo.