Categories
Habari

Mahakama yaamuru Cyprian Musiba Kulipa Fidia ya Tsh Bilioni 6 kwa Kumchafua Membe

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuamuru mwanahabari anayejitambulisha kama mwanaharakati huru, Cyprian Musiba kumlipa fidia ya Sh6 bilioni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 28,2021 na Jaji Joacquine De Mello aliyeisikiliza kesi hiyo.

Katika hukumu hiyo Musiba ametakiwa kumlipa Membe kiasi hicho cha fedha pamoja na gharama zote za uendeshaji wa kesi kwa zaidi ya miaka miwili.

Pia imeweka zuio la kudumu kwa Musiba la kutokumkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake.