Categories
Habari

Janga La Moto Mlima Kilimanjaro

Image

Mlima Kilimanjaro ulio mrefu zaidi Afrika unawaka moto, sababu ya moto huo unaowaka umbali wa mamia ya mita kutoka usawa wa bahari bado hazijajuikana.

Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen nchini Tanzania, mashuhuda wamesema kuwa jitihada za wakazi wa kuuzima moto huo lakini changamoto inayokumba zoezi hilo ni umbali ambao mto huo ulipo.

Miale ya moto ilikuwa ikionekana kutoka mji wa Moshi umbali wa makumi ya kilomita kutoka eneo la mlima kulikotokea tukio hilo.

The Citizen limenukuu Taarifa ya hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro (Kinapa) ikisema kuwa moto huo ulitokea siku ya Jumapili majira ya jioni Tarehe 11 mwezi Oktoba, kisha taarifa hiyo ilithibitishwa na afisa habari wa Shirika la hifadhi la Taifa (TANAPA)Patrick Shelutete na kusema kuwa taarifa kwa kina itatolewa kuhusu tukio hilo.

CHANZO: BBC Swahili