Categories
Habari

Dhulmati: Mjane Ailalamikia CCM Kutomlipa Kodi ya Pango Kwa Miaka Mitano, Deni Lafikia Milioni 3

Mkazi mmoja wa kata ya Osunyai ,katika jiji la Arusha , Gloria Laizer ambaye ni mama mjane, amelazimika kuangua kilio hadharani kumlalamikia mpangaji wake ambaye ni chama Cha Mapinduzi CCM kata hiyo kwa kushindwa kumlipa deni la pango katika ofisi waliopanga katika kipindi Cha miaka mitano linalofikia kiasi Cha zaidi ya shilingi milioni 3.5.

Mjane huyo amesema pamoja na jitihada zote alizozifanya kudai fedha zake ikiwemo kuifunga ofisi hiyo, lakini bado hakuna jitihada zozote za yeye kulipwa fedha zake.

Akiongea kwa uchungu huku akiangua kilio hadharani alisema anachangamoto kubwa ya kusomesha watoto wake kutokana na ukosefu wa fedha na hivyo amemwomba Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais John Magufuli kumsaidia kuweza kupata madai yake .

Amesema wamefanya vikao mbalimbali na viongozi wa CCM ili kupata mwafaka wa malipo ya Kodi yake lakini amekuwa akiambulia maneno matamu yenye matumaini na mwisho wake kutolipwa kabisa.

“Hivi Mimi nimemkosema Nini mungu nimefanya makosa kupangisha nyumba yangu kwa ccm Mimi ni mjane sina mapato yoyote zaidi ya kuegemea hii Kodi ya nyumba kwani hawa CCM wanisumbue na kutaka kunidhulumu???”alisema Gloria

Aidha alifafanua kwamba waliingia makubaliano na CCM Agosti Mwaka 2015, kwamba ccm italipa kila chumba sh,60,000 Kila mwezi kwa vyumba viwili walivyokodisha .

” lakini chaajabu hadi Sasa hawakuwahi kunilipa chochote na hivyo najikuta nikishindwa kusomesha Hata watoto wangu”alisema

Akizungumzia madai hayo kwa njia ya simu Mwenyekiti wa CCM katika kata ya Osunyai Abdi Madava amekiri kuwepo kwa Deni hilo la muda mrefu , Ila alidai hana habari Kama ofisi zimefungwa kwa sababu hajaingia ofisini kwa muda mrefu.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Joseph Masawe alisema kuwa deni hilo la pango halijalipwa kwa sababu hajaletewa invoice ya madai na hivyo wasingeweza kufanya malipo bila stakabadhi ya madai.