Categories
Habari

Clouds TV na Radio Wafungiwa na TCRA kwa “Kutangaza Takwimu za Uchaguzi Ambazo Hazijathibitishwa na NEC.”

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevifungia vituo vya habari vya Clouds TV na Radio kwa siku saba kuanzia kesho Agosti 28 na adhabu ya kuomba radhi siku nzima ya leo kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni ndogo za utangazaji za Uchaguzi.

TCRA imesema kosa walilolifanya ni kutangaza takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Hii ni adhabu ya 2 ndani ya mwezi huu kwa Clouds baada ya kipindi chake cha Jahazi kufungiwa siku chache zilizopita.