Categories
Habari

CHADEMA inamtakatisha Dkt. Hosea kugombea Urais TLS?

Kwa ufupi sana

Dkt. Hosea ni moja kati ya watu wanaogombea urais wa TLS.

Aliwahi kuwa mkurugenzi mkuu wa PCCB. Katika uongozi wake serikali enzi Rais Kikwete serikali ilikumbwa na kashfa kubwa kumbwa kama EPA, Kagoda, Richmond nk.

Nimeona baadhi ya viongozi (sio chama) wakimpa promo Dkt. Hosea.

Tunataka kujua ni hao viongozi kwa utashi wao binafsi au ni chama kinamtakatisha?

Kama ni chama je, mnatumia vigezo gani kumtakatisha? Ni lini na wapi amekuwa akisimamia yale ambayo watu wenye uchungu na nchi hii wamekuwa wakisimamia?

Ni wapi na lini amewahi kuzungumzia katiba mpya?

Ni wapi amewahi kuzungumzia sheria za hovyo kandamizi kwa demokrasia?

Ni wapi amewahi kuzungumzia uchaguzi 2020 na wizi wa kura?

Na kama itakuwa utashi wa hao viongozi tunawashauri tu jitunzieni heshima.

Chanzo: Jamii Forums