Categories
Habari

Baba Askofu Benson Bagonza, PhD, Asema Kuna Watu Wamefika Kwake Wakidhamiria Kumdhuru

Askofu Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera amesema kuna watu wenye nia ovu wamefika Karagwe wakiwa na lengo la kumdhuru.
Bagonza amejijengea umaarufu kwa namna yake ya ukosoaji wa uvunjifu wa haki za binadamu na utawala bora.

“Ni kweli siko salama. Kuna watu wanatafuta kupendezesha mamlaka kwa kuchukua uhai wangu. Wamepiga kambi hapa kwetu wakitafuta namna ya kunidhuru, hawajatumwa. Wanadhani wakifanya hivyo watapata favour ya mamlaka. Niko tayari. Sitaki mbia, ” alisema Askofu Bagonza