Categories
Habari

Anayedaiwa Kutengeneza Radi Auawa na Wananchi

Katavi. Baraka Said (30) mkazi wa kijiji cha Mtisi halmashauri ya Nsimbo ameuawa na wananchi baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso na kupigwa na kitu kizito kisogoni akituhumiwa kujihusisha na ushirikina wa kutengeneza radi.

Akizungumza na wanahabari leo Januari 29, 2022 kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, Sylvester Ibrahimu amesema tukio hilo limetokea Januari 24, 2022 saa 12 jioni kijijini hapo.

Amesema wananchi hao walimtuhumu marehemu kutengeneza radi iliyompiga Anjelina Revocatus (16) mkazi wa kijiji hicho na kusababisha kifo chake wakati anatibiwa hospitali ya rufaa Mkoa wa Katavi.

“Watuhumiwa nane wamekamatwa,John Mayonjuwa, Mashaka Mathias, Sele Richard, Revocatus Reymond, Julias Dalali, Hawa Rashid, Agnes Rashid na Tausi Abdu. Upelekezi ukikamilika watafikishwa mahakamani,” amesema Ibrahimu.

CHANZO