Categories
Biashara Maisha

@moodewji aendeleza rekodi yake ya kuwa bilionea pekee wa dola (dollar billionaire) Afrika Mashariki kwa mwaka wa tatu mfululizo

Mfanyabiashara tajiri kuliko wote nchini Tanzania, Mohammed Dewji, ametajwa katika ripoti ya kampuni ya kimataifa ya utafiti ya Henleys & Partners kuwa ndiye bilionea pekee wa dola (dollar billionaire) katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mwezi Februari mwaka huu, jarida la Forbes lilimtaja Dewji, maarufu kama Mo, kuwa mfanyabishara tajiri zaidi kuliko wote nchini Tanzania na mmoja wa mabilionea wachache barani Afrika.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Mo alitajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni 1.5.

Ripoti ya Henley &Partners imeeleza kuwa Tanzania ina mamilione wa dola (dollar millionaires) 2,400 huko 1,300 kati yao wakiwa jijini Dar es Salaam.

CHANZO