Categories
Biashara Siasa

Maoni Ya Mdau “The Boss”: Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia

Hakuna kitu kinaamua siasa kama ‘wakati’.
Wanasiasa wazuri ni wale wanaojua nyakati. zinavyobadilika na kwenda na wakati uliopo.

Watanzania walikuwa wamechoshwa mno na siasa za Magufuli…na uongozi wake kiujumla..
Kubanwa Uhuru wa kuongea
Kufokewa na kukaripiwa
Kutoa matamko Kwa ukali..
Kuzungumza Peke yake..
Kutokukosolewa ..
Kukosekana Kwa mijadala na majadiliano..
Na mengi yaliyoenda na hayo..

Ujio wa Samia umebadili siasa Kwa ujumla..
Samia hafoki anaongea Kwa upole na kushawishi ..
Anazungumzia mazungumzo na mijadala..
Hazuii kukosolewa badala yake anakaribisha kukosolewa Kwa serikali yake..

Kikubwa zaidi ni Mwanamke ..
Watu wanamtazama Kwa ‘kumhurumia’..
Na kumpa ‘all benefits of the doubts’..
Na kuelewa kuwa anapambana na mfumo dume…
Watu wengi wanaju hii nchi ngumu na wanajua Samia atahangaika kuweza kumudu …still wanafarijika na ‘kurudi Kwa Uhuru wa kuongea na kukosoa’..

Sasa kama wapinzani wanafikiri siasa za kumshambulia Rais na serikali yake zinalipa bado kama enzi za JK watakuwa wanakosea sana….
Sana Sana wataonekana ‘hawana adabu’
Na wanajaribu ‘kumuonea’ ‘Rais Mwanamke’ baada ya ‘kidume ‘ JPM
‘kuwakomesha hadi wakaufyata’..

Siasa za kipindi hiki zinahitaji ubingwa wa hoja kwenye mijadala ya kistaarabu..bila
Kuwa ‘boa’ wananchi ambao walishachoshwa na Magufuli Sana Sana wanataka ‘mzunguko’ wa hela urudi kama ule wa JK….

Kuleta siasa za ulalamishi..
Siasa za uwana harakati.
Na siasa za Ku target watu na kuwashambulia bila kujua ..’role halisi’ ya hao watu ni siasa ambazo zinakuwa ‘outdated ‘ so fast…

Watu wanampenda Samia sio Kwa sababu ni kiongozi bora.. wanampenda Kwa sababu wanaona ‘nafuu inakuja’
Upinzani ukicheza siasa za kuleta ‘distraction’wakati watu wanasubiri nafuu ije ..hasira za wananchi zinaweza washukia wao…..

Siasa inaendana na nyakati.. wapinzani wanasoma nyakati??

Source: Jamii Forums