Categories
Maoni

Maoni ya Mhariri

Kabla ya yote, uongozi wa gazeti hili unapenda kutoa shukrani kwako kwa kujisajili kutumiwa nakala ya bure kila wiki. Tunapenda kukuhakikishia kuwa hutojilaumu kuchukua uamuzi huo. Pengine unaweza kuwa unajiuliza gazeti hili limekuja kufanya nini katika uwanja ambao tayari umefurika vyombo mbalimbali vya habari. Kuna sababu mbili za msingi. Ya kwanza, Habari Tanzania inakuja kuchangia […]

Categories
Habari za Kimataifa

Urusi Kuzishambulia Nchi za Magharibi?

Urusi imeishutumu Nato na Marekani kwa “kuchochea kiwango kipya cha mvutano” baada ya Marekani na Ujerumani kuwa washirika wa hivi punde kuruhusu jeshi la Ukraine kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi kushambulia maeneo ndani ya Urusi. Msemaji wa Berlin alisema Ujerumani ina imani kuwa Ukraine ina haki ya kujilinda dhidi ya Urusi, haswa kutokana […]

Categories
Habari za Kimataifa Habari za Kitaifa

Uchaguzi Mkuu Afrika Kusini na somo kwa Tanzania, hasa CCM na Wapinzani

Afrika Kusini ilipiga kura majuzi, huku baadhi ya kura zikiashiria kuwa chama tawala cha African National Congress (ANC) kinaweza kupata chini ya asilimia 50 ya kura kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30. Karibu wapiga kura milioni 28 wa Afrika Kusini waliojiandikisha walipata nafasi ya kuchagua wawakilishi katika mabunge ya kitaifa na majimbo. […]

Categories
Habari za Michezo

Video: Ujumbe Muhimu wa @moodewji kwa wana-Simba

Categories
Habari za Uchumi na Biashara

Suala la mikopo ya nje lililomng’oa Ndugai laibuka tena

Rais Samia Suluhu ameanza ziara ya siku 6 nchini Korea ya Kusini. Moja ya yanayotajwa kuwa mafanikio ya ziara hiyo ni kusainiwa kwa mkopo wenye masharti nafuu ambapo Korea ya Kusini itaikopesha Tanzania shilingi trilioni 6.51. Hata hivyo, habari ya mkopo huo imerejesha mjadala uliopelekea Spika wa zamani wa Bunge la Muungano, Job Ndugai, ajiuzulu […]

Categories
Riwaya

Riwaya: Mama Ndubwi

Utangulizi Mama Ndubwi si mwanamke mmoja. Mama Ndubwi ni wanawake wanne tofauti. Japo wawili kati yao wana watoto, hakuna mwenye mtoto anayeitwa Ndubwi. Sasa imekuwaje wote waitwe Mama Ndubwi? Usikose sehemu ya pili ya riwaya hii ya kusisimua, ambayo itaanza rasmi katika toleo lijalo la gazeti hili.

Categories
Safu ya Afya

Afya: Vitu 10 vya Kuzingatia Kuhusu Afya Yako

2. Kula mlo bora na kuepuka vyakula vyenye athari mwilini/visivyo na faida kiafya 3. Tumia mchanganyiko wa vitamini (multivitamins) 4. Kunywa maji ya kutosha 5. Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara 6. Punguza muda wa kukaa kitako 7. Pata usingizi wa kutosha 8. Epuka unywaji wa pombe kupita kiasi 9. Dhibiti hisia hasi kama […]

Categories
Habari za Ujasusi

Ushushushu ni Kazi ya Roho Mkononi: Jinsi Majasusi wa Putin Walivyomuua kwa Sumu Mwenzao Aliyejihifadhi UK

Jasusi bado anakumbuka vizuri mchanganyiko wa msisimko na uoga aliokuwa akipata udogoni kila aliposoma vitabu vya Willy Gamba [Njama, Kufa na Kupona, Kikosi cha Kisasi, Hofu]. Alifahamu mapema kuwa kazi ya ushushushu ni hatari sana. Ikawaje basi akaja kuipenda ukubwani? Ushushushu unaendelea kuwa ni moja ya taaluma hatari kabisa kwa maana ya kutembea na roho […]

Categories
Safu ya Maisha

Mfululizo wa makala zinazofundisha jinsi ya kutumia “48 Laws of Power” katika maisha yako ya kila siku: Sehemu ya Kwanza – Orodha ya Laws zote na tafsiri yake kwa Kiswahili

Tafsiri ya moja kwa moja ya 48 Laws of Power sio rahisi sana kwa sababu ya muktadha wa neno power. Lakini kwa minajili ya makala hizi, neno hilo linamaanisha zaidi mamlaka au/na nguvu. Kwahiyo, kwa Kiswahili, 48 Laws of Power inaweza kutafsiriwa kuwa “Kanuni 48 za Mamlaka/Nguvu.” Baada ya utangulizi huo, sasa twende kwenye kitabu […]

Categories
Habari za Michezo

Mo atendewe haki, akiondoka Simba itayumba

Kwa mara nyingine Simba imemaliza ligi ya soka Bara bila ubingwa. Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa timu hiyo kongwe kuambulia patupu. Mara ya mwisho Simba kuwa bingwa ilikuwa mwaka 2021. Na katika miaka yote mitatu ambayo Simba imekosa ubingwa, watani zake wa jadi, Yanga, ndio wameibuka kidedea. Kadhalika, katika misimu yote mitatu ambayo […]